Ni ipi hukumu ya mfungaji kutumia wanja na dawa za matone kwenye pua, macho na sikio?

Swali: Ni ipi hukumu ya mfungaji kupaka wanja machoni, kuweka dawa ya matone kwenye macho, masikio na pua?

Jibu: Hakuna neno kwa mfungaji kupaka wanja, kuweka dawa ya matone machoni na masikioni. Haijalishi kitu hata kama atahisi ladha kooni. Swawm yake haiharibiki. Kwa sababu sio kula wala kunywa na wala vitu hivyo havileti maana ya kula wala kunywa. Dalili zimekuja kukataza kula na kunywa. Kwa hivyo visiingizwe visivyokuwa katika maana yake. Maoni haya tuliyotaja ndio chaguo la Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) na ndio maoni ya sawa.

Kuhusu akiweka dawa ya matone puani na yakaingia kooni mwake hanamfunguza endapo amekusudia kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pea katika kupalizia. Isipokuwa tu ikiwa kama utakuwa umefunga.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/205)
  • Imechapishwa: 09/06/2017