Ni ipi hukumu ya mfungaji kunusa vitu vyenye hafuru nzuri?

Swali 421: Ni ipi hukumu ya mfungaji kunusa harufu nzuri?

Jibu: Mfungaji kunusa harufu nzuri hakuna neno. Ni mamoja yawe mafuta au uvumba. Lakini ikiwa ni uvumba asivute moshi wake. Kwa sababu moshi uko na chembechembe ambazo zinaweza kuingia mpaka tumboni na hivyo akawa ni ameiharibu funga yake kama maji na mfano wake. Ama kule kunusa tu bila ya kuvuta ule moshi mpaka ukaingia kooni mwake hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 479
  • Imechapishwa: 10/05/2019