Ni ipi hukumu ya mfungaji kukata swawm yake kwa sababu ya kiu kingi?

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuharibu swawm yake ya wajibu kwa sababu ya kiu?

Jibu: Hukumu kwa yule ambaye analazimika kufunga swawm ya wajibu, ni mamoja iwe Ramadhaan, ya kulipa, kafara au fidia, ni haramu kwake kuiharibu swawm hii. Lakini kiu kikifikia kiwango cha yeye kuchelea kupatwa na madhara au maangamivu, basi itakuwa inajuzu kwake kukata swawm na wala hakuna neno. Haijalishi kitu hata kama ni katika Ramadhaan. Endapo atafikia kiwango cha yeye kuchelea kupatwa na madhara au maangamivu, basi itakuwa inajuzu kwake kukata swawm.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/202)
  • Imechapishwa: 09/06/2017