Ni ipi hukumu ya matamshi haya?

Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwa mtazamo wenu juu ya matamshi yafuatayo:

“Allaah anajua”, “Allaah asijaalie”, “Allaah asikadirie”, “Allaah ametaka iwe” na “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi”?

Jibu: Kuhusu “Allaah anajua” ni sawa kusema hivyo lau atakuwa ni mkweli. Kuhusu “Allaah asijaalie” na “Allaah asikadirie” ni sawa kusema hivo makusudio ya kusema hivo ni kuomba usalama kutokana na mambo yenye kudhuru. Kuhusu “Allaah ametaka iwe” ikiwa anakusudia maradhi yaliyomfika, ufukara na kadhalika ni katika makadirio na matakwa ya Allaah ya kilimwengu (Kawniyyah) ni sawa.

Kuhusiana na “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi” inajuzu kusema hivyo wakati wa uhai wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama baada ya kufa kwake aseme “Allaah ndiye anajua zaidi”. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajui yanayoendelea baada ya kufa kwake.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/108)
  • Imechapishwa: 24/08/2020