Ni ipi hukumu ya limbwata katika Uislamu?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuwapatanisha wanandoa kwa kutumia uchawi?

Jibu: Hili ni haramu na wala halijuzu. Kitendo hichi huitwa “limbwata”. Ni haramu na inaweza kufikia kiwango cha kufuru na shirki. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ

“Nao wawili hao hawamfundishi yeyote mpaka waseme: “Hakika sisi ni mtihani  tulopewa, hivyo basi usikufuru.” Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe – na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi. Hakika walijua kwamba atakayechuma haya hatopata huko Aakhirah fungu lolote.” (02:102)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/177)
  • Imechapishwa: 04/06/2017