Ni ipi hukumu ya ladha na vijiti vya Siwaak kwa mfungaji?

Swali: Ni ipi hukumu ya mfungaji kutumia Siwaak pamoja na ile ladha na vijiti vidogovidogo inavyotoa?

Jibu: Kutumia Siwaak ni Sunnah. Ni mamoja iwe kabla au baada ya jua kukengeuka kutokana na ujumla wa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Siwaak ni yenye kuusafisha mdomo na inamridhisha Mola.”

Vilevile Hadiyth nyenginezo zote zilizopokelewa kuhusu Siwaak hakuna kinachofahamisha juu ya kumbagua mfungaji. Kujengea juu ya hili ni Sunnah kwa mfungaji na asiyekuwa mfungaji.

Lakini hata hivyo ikiwa anahisi ladha kwa sababu ya Siwaak au inatoa vijiti vidogovidogo haitakikani kwa mfungaji kuitumia. Sio kwa sababu ya Siwaak yenyewe. Ni kwa sababu ya kule kukhofiwa ladha au vijiti vidogovidogo hivyo visije kufika tumboni mwake. Endapo atakuwa makini, akatema ile ladha yake na vijiti hivyo kutakuwa hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/353-354)
  • Imechapishwa: 09/06/2017