Ni ipi hukumu ya kuyajengea makaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuyajegea makaburi?

Jibu: Kuyajengea makaburi ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza hilo kwa vile ndani yake kunapatikana kuwaadhimisha wafu. Sababu nyingine ni kwa vile ni njia inayopelekea makaburi haya kuabudiwa na kufanywa mungu pamoja na Allaah. Hivyo ndivyo ilivyo hali ya majengo mengi yaliyojengwa juu ya makaburi. Matokeo yake watu wakawa wanashirikisha pamoja na watu waliyomo ndani ya makaburi haya, wakaomba pamoja na Allaah, kuwaomba wafu na kuwataka uokozi ili watatue matatizo, mambo ambayo ni shirki kubwa na ni kutoka katika Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/233)
  • Imechapishwa: 04/06/2017