Ni ipi hukumu ya kuweka viwiko ardhini wakati mtu amesujudu?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka viwiko ardhini wakati mtu amesujudu?

Jibu: Hii limechukizwa na haitakikani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Unaposujudu basi weka mikono yake chini na nyanyua viwiko vyako.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake. Pia amekataza kukalia tumbo la mguu wa kushoto na kuusimamisha unyayo wa mguu wa kulia kama anavofanya mbwa. Sunnah ni kunyanyua viwiko vyake. Ni mamoja akiwa mwanamme au mwanamke. Ni mamoja swalah ni ya faradhi au ya iliyopendekezwa. Ategemee viganja vyake vya mikono wakati wa kusujudu.

[1] Ahmad (18022) na Muslim (494).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/154)
  • Imechapishwa: 24/10/2021