Swali: Ni ipi hukumu ya kutufu kwenye kaburi kama kaburi la al-Badawiy na mengineyo?
Jibu: Kutufu kwenye kaburi endapo mtu atanuia kujikurubisha kwa yule aliyemo ndani ya kaburi ni shirki. Twawaaf ni ´ibaadah ambayo anatakiwa kutekelezewa Allaah pekee. Amesema (Ta´ala):
وَلْيَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ الْعَتِيقِ
“Watufu katika Nyumba kongwe.” (22:29)
Mwenye kutufu kinyume na Nyumba ya Allaah kwa lengo la kujikurubisha kwa mwengine asiyekuwa Yeye amemshirikisha Allaah. Amemfanyia ´ibaadah asiyekuwa Allaah. Twawaaf ni ´ibaadah kama mfano wa kuweka nadhiri, kuchinja na du´aa. Mwenye kumfanyia asiyekuwa Allaah ametumbukia kwenye shirki. Ni aina ya shirki kubwa.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/AudioDir2/67880.mp3
- Imechapishwa: 20/08/2017