Ni ipi hukumu ya kutia rangi ndevu kwa hina au katam?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzitia rangi ndevu kwa hina na katam?

Jibu: Ni Sunnah. Ni Sunnah kuzitia rangi mvi. Ndio, kuna katika Maswahabah ambao hawakufanya hivo. Ni dalili inayofahamisha ya kwamba sio lazima japokuwa lililo bora ni kufanya hivo. Wanachuoni tuliokutana nao hawakutia rangi; si  Shaykh Muhammad bin Ibraahiym, wala Shaykh as-Sa´diy wala Shaykh Ibn Humayd. Hakuna katika wao waliotia rangi. Hakuna neno. Inajuzu kutotia rangi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 23/10/2017