Ni ipi hukumu ya kuswali bila ya kukimu?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali pasi na kukimu?

Jibu: Swalah inasihi bila ya kukimu. Lakini ikiwa mji mzima haukukimu itakuwa ni lazima. Ni faradhi ya kutosheleza. Akipatikana katika mji mwenye kuadhini na kukimu, kwa wengine itabaki kuwa ni jambo lililopendekezwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 02/02/2017