Ni ipi hukumu ya kusherehekea siku ya mama?


Swali: Ni ipi hukumu ya kusherehekea siku ya mama?

Jibu: Haijuzu. Waislamu hawana zaidi ya sikukuu mbili peke yake; Fitwr na Adhwhaa. Kila sikukuu kati ya hizo mbili inakuja baada ya kutekeleza nguzo ya Uislamu. Fitwr inafanywa baada ya kutekeleza nguzo ya swawm na Adhwhaa inafanywa baada ya kutekeleza nguzo ya hajj. Kuna sikukuu tu hizi mbili; hakuna nyingine mbali na hizi si ya kina mama wala kina baba. Haifai hata kusherehekea mazao ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Ni Bid´ah. Ikiwa haijuzu kusherehekea mazao ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tusemeje juu ya mazao ya mtu mwengine, walii au kiongozi? Haijuzu. Ambaye anataka kumfanyia jema mama yake amtendee wema na sio kumtengea sherehe. Halimnufaishi kitu. Ikiwa unataka thawabu mtendee wema mama yako sawa anapokuwa hai na wakati wa kufa.