Swali: Ni ipi hukumu ya kupunguza nywele zinazozidi kwenye nyusi?
Jibu: Haijuzu kukata wala kupunguza nywele zinazozidi kwenye nyusi. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kwamba amemlaani mwenye kuchonga nyusi na mwenye kuchongwa nyusi.”
Wanazuoni wamebainisha kwamba (النمص) ni kule kukata kitu katika nyusi.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/51)
- Imechapishwa: 07/08/2021