Swali: Ni ipi hukumu ya kupunguza nyusi?

Jibu: Kupunguza nyusi ikiwa ni kwa njia ya kunyofoa basi ni haramu. Bali ni dhambi kubwa. Kunaingia katika kunyoa ambako Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani yule mwenye kufanya hivo.

Ikiwa ni kwa njia ya kupunguza au kukata, ni jambo limechukizwa na wanachuoni na wengine wakalikataza na kulifanya ni katika kunyoa. Wamesema kuwa kunyoa sio kule kukwanyua peke yake. Bali wanaonelea kuwa kunyoa ni kila kule kuzibadilisha nywele ambazo Allaah hakuzitolea idhini midhali zipo usoni.

Lakini naonelea kuwa – hata kama nitasema kuwa inafaa au imechukizwa kule kuzipunguza ima kwa njia ya kuzikwanyua au kuzinyofoa – mwanamke hatakiwi kufanya hivo. Isipokuwa ikiwa kama nyusi ni nyingi kiasi cha kwamba zinateremka mpaka machoni ambapo zikawa zinamuathiri mtu katika kuona, katika hali hii hakuna neno akaondosha zile zinazomuudhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/133)
  • Imechapishwa: 30/06/2017