Swali: Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya soksi zilizo na picha ya mnyama?

Jibu: Haijuzu kufuta juu yake. Kwa kuwa kufuta juu ya khofu ni ruhusa isiyoruhusu kwa maasi. Maoni yanayosema kuwa inajuzu kupangusa juu ya kilicho cha haramu inapelekea kumsapoti mtu huyu juu ya kuvaa kilicho haramu. Kitu cha haramu ni wajibu kukikemea. Haitakiwi kusemwa ya kwamba hili linaingia katika utwezaji na hivyo inajuzu. Hili linaingia katika mavazi na kuvaa kilicho na picha ni haramu kwa hali  yoyote ile. Kwa mfano kwenye soksi kukiwa kuna picha ya simba itakuwa haijuzu kufuta juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/165)
  • Imechapishwa: 02/07/2017