Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya soksi nyepesi zinazoonyesha?


Swali: Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya soksi nyepesi zinazoonyesha?

Jibu: Miongoni mwa sharti za kufuta juu ya soksi ziwe nene na zenye kufunika. Zikiwa nyepesi zinazoonyesha na nyembamba basi haitofaa kupangusa juu yake. Kwa sababu mguu wenye hali iliyotajwa una hukumu ya kuwa wazi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/110)
  • Imechapishwa: 15/08/2021