Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya soksi na khaswa wakati wa baridi?

Swali 05: Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya soksi na khaswa wakati wa baridi?

Jibu: Mtu afute juu yake na wala hakuna neno. Ni mamoja ni zile soksi za ngozi au ni soksi za kawaida. . Ni mamoja wakati wa majira ya baridi au ni wakati wa majira ya joto. Midhali amezivaa wakati yuko na wudhuu´ na zimefunika, basi apanguse juu yake kwa muda maalum; mchana mmoja na usiku wake kwa ambaye ni mkazi, na michana mitatu na nyusiku zake kwa ambaye ni msafiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 32
  • Imechapishwa: 31/07/2018