Ni ipi hukumu ya kuongea wakati wa kukidhi haja?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuongea wakati wa kukidhi haja? Inapata kufahamika kupitia Hadiyth ya Abu Hurayrah kujuzu?

Jibu: Haitakikani kwa mtu kuongea wakati anapokidhi haja. Kuna Hadiyth ilio na maana kama ifuatavyo:

“Hawatozungumza watu wawili na wako wanakidhi haja. Kwani hakika Allaah analichukia hilo.”

Hadiyth inafahamisha juu ya uharamu. Isipokuwa wakati wa dharurah. Kwa mfano yuko anakidhi haja na ghafla akamuona kipofu anataka kuingia kwenye shimo. Katika hali hii azungumze. Vinginevyo haijuzu.

Kuhusu Hadiyth hakuna dalili inayofahamisha kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliongea na huku anakidhi haja. Ilikuwa ni baada ya kukidhi haja.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 07/07/2018