Swali: Ni ipi hukumu ya kunyoa ndevu?

Jibu: Kunyoa ndevu ni haramu. Kwa kuwa ni kumuasi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Zirefusheni ndevu na yapunguzeni masharubu.”

 Isitoshe ni kuacha kufuata mwongozo wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na badala yake mtu kufuata mwongozo wa waabudu moto na washirikina.

Mpaka wa ndevu ni nywele za usoni, taya na mashavu. Hivyo ndivyo walivyosema watu wa lugha. Bi maana kila kilichomo katika mashavu, taya na kidevu ni katika ndevu. Kukata kitu katika hizo kunaingia katika maasi pia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) amesema:

“Zirefusheni ndevu… “

“Ziacheni ndevu… “

“Zifugeni ndevu.”

Hii ni dalili inayofahamisha kuwa haijuzu kukata kitu humo. Lakini maasi yanatofautiana. Kunyoa ni dhambi kubwa kuliko kukata. Kwani huko ni kukubwa na ni uhalifu wa wazi zaidi kuliko kukata tu. Hii ndio haki. Haki ni yenye haki zaidi kufutwa. Iiulize nafsi yako ni kitu gani kinachokuzuia kuikubali haki, kuitendea kazi kwa ajili ya kumridhisha Allaah na kutafuta thawabu Zake. Usitangulize matamanio ya nafsi yako juu ya radhi za Allaah. Amesema (Ta´ala):

وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ

“Ama yule aliyekhofu kisimamo mbele ya Mola wake na akaikataza nafsi yake na matamanio, basi hakika mabustani ndio makaazi yake.” (79:40-41)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/125-126)
  • Imechapishwa: 30/06/2017