Ni ipi hukumu ya kunyanyua mikono katika Witr?


Swali: Ni ipi hukumu ya kunyanyua mikono katika Witr?

Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kunyanyua mikono katika Qunuut ya Witr. Kwa sababu ni miongoni mwa aina za Qunuut wakati wa majanga. Imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alinyanyua mikono yake wakati alipoomba du´aa katika Qunuut dhidi ya majanga. Ameipokea al-Bayhaqiy (Rahimahu Allaah) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/51)