Swali: Ni ipi kafara ya mtu mwenye kula kwa kukusudia katika Ramadhaan pasi na udhuru wa Kishari´ah?

Jibu: Ikiwa mtu alijifunguza kwa kukusudia basi ni wajibu kwake kulipa na kutoa kafara pamoja na kutubu kwa Allaah (Subhaanah). Kafara ni kuacha mtumwa huru ambaye ni muumini. Asipoweza afunge miezi miwili mfululizo. Asipoweza alishe masikini sitini. Hayo yanamuhusu pia mwanamke midhali amefanya pasi na kutenzwa nguvu.

Ikiwa amejifunguza kwa kula, kunywa na mfano wa hayo, basi ni wajibu kwake kulipa na kufanya tawbah. Lakini hata hivyo haimlazimu kutoa kafara.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/355)
  • Imechapishwa: 22/06/2017