Ni ipi hukumu ya kula au kunywa chooni?

Swali: Ni ipi hukumu ya kula au kunywa chooni?

Jibu: Chooni ni mahali pa kukidhia haja peke yake. Haitakikani kubaki ndani yake isipokuwa kwa kiasi cha haja tu. Mtu kujishughulisha na kula na kunywa ndani yake kunapelekea kubaki huko kwa muda mrefu, jambo ambalo halitakikani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/110)
  • Imechapishwa: 14/06/2017