Swali: Ni ipi hukumu ya kujipaka wanja?

Jibu: Kujipaka wanja kumegawanyika sehemu mbili:

Ya kwanza: Mtu akatumia wanja kwa ajili ya kuyafanya macho yawe na nguvu, yaone vizuri na kuyasafisha. Nia sio kuyapamba. Hili halina neno. Bali ni miongoni mwa mambo yanayotakiwa kufanywa. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akijipaka wanja kwenye macho yake. Hili ni khaswa pale ambapo wanja huu utakuwa ule wa asili [alokuwa akitumia Mtume].

Ya pili: Mtu akusudie kujipamba na kujipodoa. Haya ni kwa wanawake. Mwanamke anatakiwa ajipambe kwa ajili ya mumewe.

Kuhusu wanaume ni jambo linalotakiwa kutazamwe vizuri. Mimi nakomeka. Lakini hata hivyo kunaweza kutofautishwa kati ya kijana ambaye kunakhofiwa juu yake fitina, akatazwe, na kati ya mtumzima ambaye hakukhofiwi juu yake fitina, asikatazwe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/116)
  • Imechapishwa: 16/06/2017