Ni ipi hukumu ya kufunika kichwa ndani ya swalah?

Swali: Ni ipi hukumu ya kufunika kichwa ndani ya swalah?

Jibu: Ni lazima kwa mwanamke kufunika kichwa chake. Kwa sababu mwili wa mwanamke wote hautakiwi kuonekana isipokuwa tu uso wake ikiwa karibu naye hakuna wanaume ajinabi. Karibu naye kukiwa kuna wanaume ajinabi basi anatakiwa kufunika pia uso wake. Kuhusu mwanaume akifunua kichwa chake hakuna neno. Lakini kule kuswali akiwa katika muonekano mzuri ndio bora zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 09/03/2019