Ni ipi hukumu ya kufunga siku ya idi?

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu aliyefunga siku ya ´iyd pamoja na kuwa anajua kuwa ni siku ya ´iyd?

Jibu: Haijuzu kufunga siku ya ´iyd kutokana na Hadiyth Swahiyh zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zinazokataza kufunga siku ya ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhwhaa. Wanachuoni wameafikiana juu ya uharamu wa hilo. Ni wajibu kwa yule aliyefanya hivo kutubia kwa Allaah (Subhaanah) na asirudi tena kufanya hivo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/214)
  • Imechapishwa: 09/06/2017