Ni ipi hukumu ya kufumba macho wakati wa kuswali?

Swali: Ni ipi hukumu ya kufumba macho wakati wa kuswali?

Jibu: Kufumba macho ndani ya swalah ni jambo limechukizwa. Kwa sababu ni jambo linakwenda kinyume na yale aliyokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Isipokuwa kukiwa kuna sababu. Kwa mfano kwenye ukuta au kwenye godoro kuna mapambo au mbele yake kuna mwangaza mkali wenye kuudhi macho yake. Kwa hali yoyote ni kwamba hapana neno ikiwa kuna sababu iliyomfanya yeye kufumba macho. Vinginevyo ni jambo limechukizwa. Anayetaka faida zaidi basi arejee katika kitabu “Zaad-ul-Ma´aad” cha Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 341
  • Imechapishwa: 09/05/2020