Ni ipi hukumu ya kufanya sikukuu za kuzaliwa au sikukuu ya ndoa?


Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya sikukuu za kuzaliwa au kwa mnasaba wa ndoa?

Jibu: Katika Uislamu hakuna sikukuu mbali na sikukuu ya wiki ambayo ni siku ya ijumaa, sikukuu ya siku za mwanzo za Shawwaal ambayo ni ´Iyd-ul-Fitwr na sikukuu inayofanywa katika zile siku kumi za Dhul-Hijjah ambayo ni ´Iyd-ul-Adhwhaa. Mtu anaweza vilevile kuita ile siku ya ´Arafah kuwa ni sikukuu kwa wale walioko ´Arafah na yale masiku ya kuchinja yanayofuatia baada ya ´Iyd-ul-Adhwhaa.

Kuhusu sikukuu za siku ya kuzaliwa kwa ajili ya mtu, watoto, sikukuu kwa mnasaba wa ndoa na nyenginezo zote hazikuwekwa katika Shari´ah. Ziko karibu zaidi na uzushi kuliko uruhusikaji.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/302)
  • Imechapishwa: 09/06/2017