Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya kazi pamoja na makafiri? Unaninasihi nini?

Jibu: Namnasihi ndugu huyu ambaye anafanya kazi pamoja na makafiri atafute kazi nyingine ambapo ndani yake hamna yeyote katika maadui wa Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao wanaamii dini nyingine mbali na Uislamu. Ikiwa kuna wepesi kufanya hivo basi hilo ndilo linalotakikana. Isipokuwa rahisi kufanya hivo hakuna dhambi juu yake. Yeye afanye kazi yao na wao wafanye kazi zao. Lakini kwa sharti kusiwe ndani ya moyo wake kuwapenda na kuwafanya marafiki. Anatakiwa vilevile kushikamana na yale yaliyokuja na Shari´ah kutokamana na yale yanayohusiana na Uislamu, kuwaitikia salamu na mfano wa hayo. Jengine ni kwamba haifai kulifuata jenezao lao, kuhudhuria mazishi yao, wala asishuhudie sherehe zao na wala asiwapongeze kwazo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/40)
  • Imechapishwa: 06/06/2017