Ni ipi hukumu ya kuchelewesha swalah kwa ajili ya kazi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuchelewesha swalah kwa ajili ya kazi?

Jibu: Ikiwa ucheleweshaji ni mpaka mwisho wa wakati wake tu lakini hata hivyo akawa ameswali ndani ya wakati wake hakuna neno. Kwa sababu kuitanguliza swalah katika ule wakati wake wa kwanza ni bora na sio wajibu. Hapa ni pale ambapo kutakuwa hakuswaliwi swalah ya mkusanyiko msikitini. Vinginevyo itakuwa ni wajibu kwake kuhudhuria swalah ya mkusanyiko. Isipokuwa ikiwa kama yuko na udhuru.

Ama ikiwa ucheleweshaji huu unaitoa nje ya wakati wake ni jambo lisilojuzu. Isipokuwa ikiwa kama mtu atasahau na akafanya kazi sana mpaka mpaka wakati ukatoka. Mtu kama huyu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayelala na kupitwa na swalah au akasahau basi na aiswali pale atapokumbuka.”

Huyu anatakiwa kuswali pale tu atapokumbuka na hana dhambi. Ama mtu akumbuka swalah lakini hata hivyo kutokana na kazi hii ambayo inamshughulisha dunia yake kutokamana na Aakhirah yake ni haramu na wala haijuzu. Hata kama ataiswali baada ya wakati wake kutoka haitokubaliwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema yule ambaye atachelewesha swalah mpaka nje ya wakati wake pasi na udhuru wa Kishari´ah basi swalah yake haisihi. Kwa sababu ameitoa nje ya wakati ambao ameamrishwa kuitekeza pasi na udhuru. Katika hali hiyo anakuwa ametenda kitendo ambacho hakukiamrisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/32)
  • Imechapishwa: 06/06/2017