Ni ipi hukumu ya kuchelewesha ´Ishaa?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuchelewesha swalah ya ´ishaa na kuiswali sehemu ya mwisho ya usiku?

Jibu: Bora katika swalah ya ´ishaa ni kuichelewesha kiasi mtu atakavyoweza. Kila ambavyo mtu ataichelewesha ndio bora zaidi. Lakini ikiwa kuchelewesha kutapelekea kukosa swalah ya mkusanyiko, basi katika hali hiyo haitofaa kuichelewesha na kupitwa na swalah ya mkusanyiko.

Kuhusu wanawake majumbani, kila ambavo watachelewesha swalah ya ´ishaa ndio bora kwao. Lakini hata hivyo wasiicheleweshe mpaka katikati ya usiku.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/211)
  • Imechapishwa: 17/07/2020