Swali 08: Ni ipi hukumu ya kubadilisha nia katika swalah ya sunnah? Kwa mfano mtu anaswali Tahiyyat-ul-Masjid na akabadilisha nia na kunuia kwamba ni swalah ya sunnah ya kabla [ya Dhuhr]?

Jibu: Asibadili nia. Ni lazima kwa mtu kukamilisha kile alichonuia. Isipokuwa atapotaka kuswali swalah ya sunnah ambapo kukakimiwa swalah kabla ya kumaliza Rak´ah ya pili na kabla ya Rukuu´ ya pili. Katika hali hii basi aikate na kuibatilisha. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kukikimiswa swalah basi hakuna swalah isipokuwa ile ya faradhi.”[1]

Ama kusema kwamba abadilishe kutoka Tahiyyat-ul-Masjid na kwenda Raatibah na yeye yuko katikati ya swalah, asifanye hivo. Kuianza nia kwa yeye kunuia kuanzia mwanzoni mwa swalah akanuia hiyo Raatibah ni sawa. Ama yeye hakunuia mwanzoni mwa swalah na akaingia ndani ya swalah akiwa na nia ya kuswali Tahiyyat-ul-Masjid hakunufaishi kitu kuifanya upya katikati ya swalah. Isipokuwa akiikata na akanuia upya.

[1] Muslim (710).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 33
  • Imechapishwa: 20/09/2018