Ni ipi hukumu ya kikao cha mapumziko?

Swali 24: Ni ipi hukumu ya kikao cha mapumziko1 (جلسة الاستراحة)?

Jibu: Kimependekezwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikikaa. Baadhi ya wanachuoni wengine wanasema kuwa hakikupendekezwa kwa sababu huenda (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo kwa sababu ya uzito wake au kwa sababu ya kuchoka. Lakini maoni yaliyo na nguvu ni kwamba kimependekezwa.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/66-kikao-cha-kupumzika/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 36
  • Imechapishwa: 01/11/2018