Ni ipi hukumu ya ´Awwaam wa Shiy´ah na Suufiyyah?

Swali: Watu wasiokuwa na elimu wa Shiy´ah na Suufiyyah wahukumiwe kuwa ni makafiri?

Jibu: Wanawafuata mabwana wao. Ikiwa wanaamini kama wanavyoamini wao basi ni wenye kuwafuata.

Swali:  Wako ambao wanawatetea Raafidhwah kwa sababu ya kujahili madhehebu yao. Wanaponasihiwa wanasema kuwa sisi ni wenye ushabiki (Ta´ssub).

Jibu: Muwekee wazi I´tiqaad zao. Kuwanasihi sio ushabiki. Mfano wake ni kama ambaye anamtetea Ibn Abiy Rabiy´ah. Wabainishie ni ipi I´tiqaad zao na kwamba wamechupa mipaka kwa ´Aliy na wanawaomba msaada watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio ´Aqiydah yao. Wao ni kama makafiri wa Quraysh ambao walikuwa wakiwataka msaada kina al-Laat, al-´Uzzaa, Manaat, Habl na masanamu ambayo wanayatekelezea ´ibaadah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 83-84
  • Imechapishwa: 09/07/2019