Ni ipi hukumu ya ambaye anambashiria mwenzie Pepo?

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anambashiria mwenzie Pepo?

Jibu: ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawamshuhudilii yeyote Pepo. Hashuhudiliwi isipokuwa yule aliyeshuhudiliwa na maandiko kama wale kumi walioahidiwa Pepo, al-Hasan na al-Husayn ambao ni viongozi wa vijana wa Peponi na Bilaal (Radhiya Allaahu ´anhum). Vinginevyo faida itakuwa iko wapi kuwashuhudilia watu tu Pepo? ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawamshuhudilii muislamu yeyote Moto. Lakini hata hivyo wanamtarajia vyema yule mwema na wanachelea juu ya mtenda dhambi. Mtu mwema ambaye amenyooka katika kumtii Allaah kunamtarajia kheri. Mtenda maasi tunachelea juu yake Moto. Pamoja na hivyo inatakiwa kushuhudia kwa jumla kwamba kila muumini ataingia Peponi kama ambavyo kila kafiri ataingia Motoni. Ama kulenga mtu fulani haifai. Hatujui hali yake. Haya ndio maoni ya wanachuoni wengi na ndio ya sawa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 05/02/2018