Swali: Ni ipi hukumu mtu akiota katikati ya Ihraam yake? Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Mtu akiota katikati ya Ihraam yake na akatokwa na manii basi ni lazima kwake kuoga na hana jengine juu yake. Ihraam yake ni sahihi na wala haimdhukuru kitu. Kwa sababu hakufanya hivo kwa kutaka kwake. Kadhalika swawm katika Ramadhaan na miezi mingine mtu akiota swawm yake ni sahihi. Lakini akitokwa na manii atatakiwa kuoga joshi la janaba.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15152/%D9%87%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AD%D8%AA%D9%84%D8%A7%D9%85-%D9%8A%D9%81%D8%B3%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AD%D8%B1%D8%A7%D9%85
  • Imechapishwa: 17/08/2018