Swali: Ni ipi hukumu mfungaji kumeza mate?

Jibu: Hakuna neno kumeza mate. Sijui kama kuna tofauti yoyote juu ya hilo wanachuoni kutokana na ule uzito na ugumu wa kujiepusha na hilo.

Kuhusu makohozi[1] ni lazima kwa mtu kuyatema pale yanapofika kinywani. Haijuzu kwa mfungaji kuyameza kwa sababu kuna uwezekano wa kuyaepuka tofauti na mate.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/damu-inayotoka-katikati-na-meno-wakati-wa-swawm-na-hukumu-ya-mate-na-makohozi/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/313)
  • Imechapishwa: 01/06/2018