Ni ipi hukumu kwa mgonjwa ambaye amefunga kufanya enema?


Swali: Ni ipi hukumu kwa mgonjwa ambaye amefunga kufanya enema?

Jibu: Enema ambayo mgonjwa anaingiza kidude kwenye tupu ya nyuma wanachuoni wametofautiana. Kuna wanachuoni wenye kuonelea kuwa kinafunguza kwa kujengea ya kwamba kila ambacho kinafika kooni kinaharibu swawm. Wanachuoni wengine wakasema kuwa hakifunguzi. Mingoni mwa wanachuoni wenye maoni hayo ni Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah). Sababu alotoa ni kwamba huku sio kula wala kunywa na wala hakuleti maana ya kula wala kunywa.

Naonelea kwamba inatakiwa kutazama maoni ya madaktari. Wakisema kuwa enema ni kama kula na kunywa, basi itakuwa ni jambo lenye kufunguza. Wakisema enema haiupi mwili yale yanayoupa kula na kunywa, basi itakuwa ni jambo lisilofunguza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/204)
  • Imechapishwa: 09/06/2017