Ni ipi hukumu kwa asiyejua masharti ya Shahaadah?

Swali: Ni ipi hukumu ikiwa mtu hakufanya masharti saba ya “Laa ilaaha illa Allah”?

Jibu: Ikiwa anaamini maana yake [ni sawa] hata kama hajui masharti yake. Ambaye si msomi anaweza kutokujua masharti. Muhimu ni kuwa anamwamini Allaah peke yake na kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba vyote badala yake ni batili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 102
  • Imechapishwa: 03/01/2017