Ni ipi hekima ya kurefusha kisimamo cha usiku?


Swali: Ni ipi hekima baadhi ya Rakaa´ katika yale masiku kumi ya Ramadhaan  ni ndefu katika kisomo chake, Rukuu´ zake, Sujuud zake na baadhi ya zengine ni fupi?

Jibu: Hakuna katika hayo Sunnah sahihi inayofahamisha juu ya hilo kwa ufafanuzi. Lakini watu wamezowea hilo kwa sababu ya kuwafanyia wepesi watu na kuwapendezea ili waweze kusimama usiku. Kwa hivyo yule mwenye kukhafifisha au kurefusha hakuna neno. Hayo yanaweza kufanywa sehemu ya mwanzo ya usiku au sehemu ya mwisho ya usiku. Sambamba na hilo inatakiwa kwa mtu kuchunga ule uwazi wa kisomo na kuwa na unyenyekevu ndani yake. Pamoja vilevile na kuwa na utulivu katika swalah na kutofanya haraka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/45-46)
  • Imechapishwa: 07/06/2018