Ni ipi hekima ya kubadili njia siku ya ´Iyd?

Swali: Ni ipi hekima ya kubadili njia siku ya ´Iyd?

Jibu: Hekima vile ninavoona:

Mosi: Kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ni Sunnah.

Pili: Miongoni mwa hekima vilevile ni kudhihirisha nembo ya swalah ya ´Iyd  katika masoko yote yaliyoko katika mji.

Tatu: Miongoni mwa hekima vilevile ni kwamba mtu anapata kuwaona wale mafukara na wengine walioko kwenye masoko.

Nne: Miongoni mwa hekima vilevile ni kwamba njia mbili zitamshuhudia siku ya Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/237)
  • Imechapishwa: 14/06/2018