Ni idadi ipi ya juu kabisa na ya chini ya Tasbiyhaat katika swalah?

Swali 19: Wapo baadhi ya wanachuoni wanaosema kwamba idadi ya Tasbiyhaat ambazo ni wajibu ni moja tu. Unasemaje juu ya hilo? Ni idadi ipi ya juu kabisa?

Jibu: Idadi ya chini kabisa ni moja. Huu ndio msingi. Akisema moja basi atakuwa ametekeleza Tasbiyh. Hata hivyo hakuna idadi ya juu kabisa. Lakini Anas (Radhiya Allaahu ´anh) alihesabu Tasbiyhaat za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba zilikuwa kumi[1]. Mtu akisabihi mara tano au saba jambo hili ni pana. Hata hivo lililo bora mtu asipunguze chini ya tatu.

[1] Abu Daawuud (888), an-Nasaa’iy (1137), Ahmad (12661) na al-Maqdisiy katika ”al-Mukhtaarah” (1/146). Nzuri kwa mujibu wa an-Nawawiy katika ”Khulaaswat-ul-Ahkaam” (1/414).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 35
  • Imechapishwa: 09/10/2018