Ni haramu kumsengenya mtu mbaya?


Swali: Kuna mtu ambaye shari yake imeenea kwa kuwaudhi watu na mfano wa hayo. Je, ni haramu kumsengenya?

Jibu: Ndio, ni haramu kumsengenya. Ni kwa nini umtaje na umsengenye? Mwache kwa vile Allaah amekusalimisha naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 10/02/2018