Swali: Nimesikia kwa baadhi ya watu wanasema kwamba haifai kwa mtu kukata kucha zake katika yale masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah. Je, niliyosikia ni kweli?

Jibu: Ikiwa anataka kuchinja basi haifai kwake kukata kucha zake, nywele zake wala chochote katika mwili wake mpaka pale atapochinja baada ya kuingia mwezi. Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Utapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah na akataka mmoja wenu kuchinja, basi asichukue/asikate kutoka katika nywele zake, kucha zake wala ngozi yake kitu chochote.”

Ama ikiwa hatochinja hakuna ubaya. Anaweza kukata katika Dhul-Hijjah na miezi mingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12640/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%82%D8%B5-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B8%D9%81%D8%A7%D8%B1-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D8%B4%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%88%D9%84-%D9%85%D9%86-%D8%B0%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%AC%D8%A9
  • Imechapishwa: 17/08/2018