Ni haramu kuhifadhi picha, sembuse kuzitundika

Swali: Watu wengi wanachukulia wepesi picha za kivuli. Baadhi wanazihifadhi kwa ajili ya kumbukumbu, wengine wanazitundika. Tunaomba utubainishie jambo hili.

Jibu: Naona kuwa kuhifadhi picha kwa sababu ya kumbukumbu ni haramu. Kwa sababu ni jambo linaloingia ndani ya ujumla wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Malaika hawaingii nyumba kuliko ndani picha wala mbwa.”

Kuzitundika ni haramu zaidi. Kuzitundika kunapelekea kuziadhimisha. Kwa ajili hii utawaona wale ambao wanawatukuza baba zao, ndugu zao au waalimu zao wanatundika picha zao sebuleni. Hapana shaka kwamba ni haramu.

Lakini yule anayehifadhi picha kwa sababu ya haja kama vile kitambulisho au leseni au anadhani kuwa ataihitajia picha hii katika mustakabali, hapana neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (150 B) Dakika: 11.34
  • Imechapishwa: 02/07/2021