Ni hali zipi ambapo mtu anasujudu Sujuud ya kusahau kabla ya Tasliym na baada ya Tasliym?

Swali 28: Ni hali zipi ambapo mtu anasujudu Sujuud ya kusahau kabla ya Tasliym na baada ya Tasliym?

Jibu: Sujuud ya kusahau inasujudiwa kabla ya Tasliym isipokuwa tu katika hali mbili:

1- Pale atapotoa Tasliym mapema kwa kupunguza Rak´ah moja au zaidi. Katika hali hii bora ni kuileta baada ya Tasliym. Dalili ya hilo ni Hadiyth ya Dhuul-Yadayn (Radhiya Allaahu ´anh).

2- Pale ambapo mtu atakuwa na dhana yenye nguvu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atapokuwa na mashaka mmoja wenu juu ya swalah yake, basi ajibidishe juu ya lile la sawa, akamilishe kitendo chake, kisha alete Tasliym na kusujudu Sujudu mbili.”[1]

Ameifanya Sujuud kuwa baada ya Tasliym. Hili ndio bora. Vinginevo Sujuud ya kusahau mtu anaileta kabla ya Tasliym.

[1] al-Bukhaariy (401) na Muslim (572).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 36
  • Imechapishwa: 02/11/2018