Ni haki wa walii kumpeleleza mposaji


Swali: Kuna mtu amepewa mtihani wa kutumia madawa ya kulevya. Allaah akamjaalia kuweza kuachana na maradhi haya na sasa yuko katika kipindi cha matibabu ya mwisho na anataka kuoa. Je, ni lazima kwangu kumweleza anayetaka kumuoa na mzazi wake kuwa anatumia mambo haya?

Jibu: Ndugu! Yule anayeolewa msichana wake na walii wake ndiye ambaye ana haki ya kumuuliza mposaji. Yeye ndiye ana haki ya kumuuliza mposaji. Wewe usiwaambie kitu. Ama kuhusu swali, hii ni haki yao wao ndio wana haki ya kumuuliza na kumpeleleza anayemjua n.k.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fth-mjd-01061435-01.mp3
  • Imechapishwa: 19/09/2020