Swali: Unasemaje juu ya ambaye anamaliza mazoezi ya michezo – ni mamoja awe askari au asiwe askari – kwa kusema “Allaah”, Allaah”, “Allaah”? Je, kufanya hivo kuna kujifananisha na Suufiyyah?

Jibu: Hii sio Dhikr. Kusema “Allaah”, “Allaah” na “Allaah” ni miongoni mwa Adhkaar za Suufiyyah. Aseme “Allaahu Akbar”, “Subhaan Allaah na  “Alhamdulillaah”. Neno hili ni miongoni mwa Adhkaar za Suufiyyah. Hazifidishi moyoni imani wala yakini. Ni lazima kuongeza juu yake sentesi nyingine ili iwe sentesi yenye kufidisha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 21/11/2021