Swali: Baba yangu alinisaidia mimi na mmoja katika ndugu zangu katika kuoa. Kuhusu ndugu zangu wengine vile ninavoamini ni kuwa wana uwezo na wala hawakumuomba kitu. Wao hivi sasa wanasema kuwa kule baba yetu kutusaidia ni deni juu yetu.

Jibu: Maneno haya kuwa kule baba kumsaidia wake fakiri kwamba ni deni juu yake ni ya batili. Hayana usahihi wowote. Mtu kumsaidia mtoto wake kunaingia katika kumpa matumzi kwa wema. Wao Allaah amewatajirisha na hawakuwa na haja ya kuozwa na baba yao.

Kujengea juu ya haya endapo mtu atakuwa na mtoto aliye na miaka ishirini ambaye anahitajia kuoa na mtoto mwengine ana miaka kumi ambaye hahitajii kuoa, akamuoza yule wa kwanza na asimpe chochote yule wa pili – hapa atakuwa ametenda haki kati ya watoto wake? Jibu ni ndio. Amefanya uadilifu. Zile pesa alizomuoza mtoto mkubwa sio deni kwake. Zinaingia katika matumizi aliyompa baba ambayo analipwa thawabu na ujira kwayo. Kule kumpa mtoto wako matumizi ni swadaqah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Sa´d bin Abity Waqqaas:

“Tambua kuwa wewe hutotoa matumizi yoyote ambayo kwayo unatafuta Uso wa Allaah isipokuwa utapewa ujira kwayo mpaka kile unachokiweka kinywani kwa mwanamke wako.”

Mpaka kile mtu anachoweka kinywani kwa mke wako analipwa thawabu kwacho midhali anatafuta Uso na radhi za Allaah.

Baba si mwenye kupata dhambi kwa kumuoza mtoto wake ambaye ni fakiri na akaacha kuwaoza watoto wake ambao ni matajiri. Yule mtoto aliyeozwa hana deni.

Tumebakiza kusema: Je, inajuzu kwa baba kuacha anausia wapewe watoto wake wadogo ambao bado hawajafikisha umri wa kuoa katika uhai wake kiwango kile cha pesa alichomuozesha kwacho mtoto wake mkubwa ambaye alikuwa fakiri? Jibu ni hapana haifai. Ni tofauti na vile wanavyoelewa baadhi ya watu. Anapowaoza watoto wake wakubwa basi anausia watoto wadogo wapewe kiwango kilekile alichomuoza yule mkubwa. Hili ni kosa. Wasia huu hautakiwi kutekelezwa. Kile kiwango alichoacha anausia wapewe watoto wake wadogo waoe kwacho kinatakiwa kuwekwa katika pesa za mirathi na zigawanywe kwa mujibu wa Shari´ah ya Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/781
  • Imechapishwa: 15/01/2018