Ngazi ya ukweli mno ni kwa Maswahabah pekee?

Swali: Ngazi ya kuwa mkweli mno (الصديقية) ni maalum kwa Maswahabah? Ni vipi mtu anaweza kufikia katika ngazi hii?

Jibu: Hapana, si maalum kwa Maswahabah. Ngazi ya kuwa mkweli mno imeenea:

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ م مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا

“Na atakayemtii Allaah na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii na wakweli na mashahidi na [waja] wema – na uzuri ulioje hao kuwa ni rafiki [zake].”[1]

Hata hivyo Maswahabah ni bora kuliko wengine. Hakuna yeyote awezaye kuwa sawa na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).

[1] 04:69

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (72) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighassat%20-11-01-1439h.mp3
  • Imechapishwa: 16/12/2017