Nende kusoma dini au nibaki na mama?


Swali: Mama yangu hataki kuniacha nende katika mji mwingine kusoma. Baada ya kumnga´ang´ania mwishoni akanikubalia. Hata hivyo najua kuwa kwa ndani hataki. Nisafiri nende kutafuta elimu au nibaki naye? Pamoja na hivyo katika wilaya yetu kuna chuo kikuu kisichokuwa cha Kishari´ah.

Jibu: Ikiwa anakuhitajia baki naye. Hili ni bora kuliko kusoma. Ni wajibu wako kumhudumikia na kuwa mzuri kwake.

Ama ikiwa hakuhitajii au hakuwekei uzito wa kusoma, usimtii katika hilo. Ni dhambi kusoma. Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba. Jaribu kufahamiana naye na kumshawishi. Akikukubalia usianze kupekua anavyohisi kwa ndani. Allaah peke yake ndiye anajua yaliyomo ndani ya moyo wake. Akikukubalia inatosheleza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 09/06/2018